Na Mwandishi wetu maalumu
VIONGOZI, wachezaji wa timu ya Yanga African na uongozi wa
hoteli ya Smart ambayo hiyo ilikuwa imefikia ilipokuwa mkoani Kagera kucheza
ligi kuu ya vodacom na timu ya Kagera sugar wamepinga vikali taarifa zilizochapishwa kwenye moja ya chombo vya habari.
Kwa nyakati tofauti wakati wakiongea na vyombo mbalimbali
vya habari vilivyoko mkoani Kager wamesema sio kweli kwamb wachezaji wa timu
hiyo uongozi uliwalaza mzungu wa nne
yaani chumba kimoja kwa wachezaji wa nne.
Walisema taarifa hizo sio sahihi kuwa zinalenga kuugawa
uongozi wa timu hiyo na washabiki wake pamoja na wanachama, kiongozi wa msafara wa timu hiyo Tito Osollo
aliwaambia waandishi wa habari kuwa chumba kimoja kilikuwa kinatumiwa na
wachezaji wawili tu.
“Walioandika habari hizi wanatumiwa haiwezekani mwandishi
akaandika habari kuwa sababu za timu ya Yanga kufungwa na Timu ya Kagera Sugar
kwamba zimechangiwa na wachezaji wane kulala chumba kimoja” alisema.
“Mwandishi aliyeandika habari hizi hafai kabisa ni mwongo na
ninawaomba wanachama na mapenzi ya timu ya Yanga kumpuuza , hayuko makini na
kazi yake hivyo anafanya kazi kwa matakwa ya wanaomtumia” alisema Osollo kwa
hasira.
Alisema Club ya yanga kamwe haitawavumulia waandishi
wanaotaka kuchonganisha wachezaji, wapenzi, wanachama na viongozi wa timu hiyo,
“ Tumefungwa, unaposhindana tegemea mambo mengi kushinda, kushindwa na kutoka
sare” alimaliza.
Kutokana sakata hilo
meneja wa hoteli ya Smart ameahidi
kumfikisha mwandishi wa habari aliyeandika habari za upotoshaji kuwa wachezaji
wa nne wa timu ya Yanga walikuwa wanalala ndani ya chumba kimoja.
“Nimeishawasiliana na mwanasheria wetu tunaandaa hati ya
madai, mwandishi huyu nitamdai fidia ya shilingi bilioni 2 , ameidhalilisha
hoteli yangu, sasa namshughulikia ipasavyo, nitamshtaki kama
yeye sio chombo, chomo hakikumtuma aandike habari za uongo” alisema kwa
msisitizo.
Nao wachezaji wa yanga walioongea kwa nyakati tofauti
walikanusha taarifa hizo kwa kusema kuwa uongozi wa klabu ya Yanga haukuwalaza
wachezaji wane kwenye chumba kimoja.
No comments:
Post a Comment