Mashabiki wa klabu ya Zenit St
Petersburg inayoshiriki katika ligi kuu ya premier nchini Urussi,
wametoa wito kwa wasimamizi wa klabu hiyo kutowasajili wachezaji weusi
na wale wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja.
Kundi kubwa zaidi la mashabiki wa klabu hiyo
maarufu kama ''Landscrona'' limesema kuwa klabu hiyo limelazimishwa
kuwasajili wachezaji weusi.
Wamesema, wachezaji ambao wanashiriki katika mapenzi ya jinsia moja, ni aibu kwa mji wao ambo una heshima zake.
Lakini mkurugenzi wa klabu hiyo wa masuala ya
michezo, Dietmar Beiersdorfer,amesema wachezaji wa klabu hiyo husajiliwa
bila kuzingatia mahala au nchi wanakotoka,rangi au dini wanayoshiriki.
Hata hivyo klabu hiyo ya Zenit, imethibitisha kuwa inafahamu umuhimu wa uvumilivu.
Hadi mwanzo wa mwaka huu, klabu ya Zenit ndiyo
iliyokuwa klabu ya pekee inayoshiriki katika ligi kuu ambayo haikuwa na
mchezaji mweusi.
Mapema mwaka huu klabu hiyo Zenit walimsajili
mshambulizi Hulk kutoka Brazil na mcheza kiungo kutoka Ubelgiji Alex
Witselfor kwa kitita cha pauni milioni 64.
Mcheza kiungo cha wa Ufaransa Yann M'Vila
aliripotiwa kukataa uhamisho hadi klabu hiyo mwezi Agosti mwaka huu
kutokana madai ya ubaguzi wa rangi.
BBC/SWAHILI
No comments:
Post a Comment