Tuesday, December 11, 2012

WAKAZI WA MKOA WA KAGERA WALIVYOPOKEA BASI JIPYA LA KAMPUNI YA FRIENDS BUS SERVICE LEO HII BUKOBA. NI MAMBO YA BUKOBA MILK LEO!

Wakazi wa Mkoa wa Kagera leo walijitokeza kupokea busi jipya la Friends safari kwa ajili ya safari za Bukoba -Kampala.

Kampuni hiyo ya FRIENDS imeleta basi hilo kuongeza nguvu na pia imeongeza uboreshaji wa safari zake za kila siku kwenda Kampala na Kurudi Bukoba. Pia imeweza kuongeza safari za Kampala - Bukoba - Mwanza. Hivyo wakazi wa Mkoa wa Kagera watanufaika na usafiri wa mabasi hayo wa Friends kwa kusafiri salama na kwa uhakika  Siku hadi siku kwenda na kurudi.

Ndani ya basi kuna TV ya kisasa "Led' HD" pamoja na mziki safi, Huduma mbalimbali kama maji, n.k 
pia huduma ya kwanza kama abiria atakuwa anajiskia vibaya watoa huduma watamfikia mara moja ndani ya basi hizo zinazosafiri kila siku. kwa usafiri wa uhakika tumia mabasi ya Friends.
Eneo la Stendi kuu leo hii
Niliweza kwenda eneo la mbali ya mji, nikakuta wananchi waliokuwa wamepewa taarifa ya ujio wa basi hilo na hapa wadau mbalimbali wakiwa wanalisubiri kwa ham.
Muda si muda basi lenyewe likawafikia..
Mwonekano wa basi lenyewe kwa nyuma
Hapa dreva alilazimika kulisimamisha basi hilo kusalimiana na Wananchi waliokuwa eneo hilo
Safari ikielekea Bukoba mjini ...


Wakazi wakilishangaa basi likiingia langoni standi
Basi likikatiza eneo la Raundi About kuingia Standi kuu
Abiria wakishuka eneo la standi
Wadau wakichungulia basi lenyewe hapa....Da! da ....
Kushoto ni Bw.Charles akiwa na hamu na shauku kubwa kuliona basi hilo maeneo ya Standi
Dreva Natukunda aliyelileta basi hilo lenye namba UAS 950M
Ndani ya basi maeneo ya Screen .... walikuwa wanaangalia movie kali ya kichina ..
Nje sasa ..Dreva akipongezwa kwa kufika salama na abiria wake na Dreva Ndugu Abdallah
Ndugu Natukunda (kulia) akipongezwa kwa kufika salama na Bw. Yusuph Songoro baada ya kufika mjini  Bukoba
Bw. Yusuph Songoro (kushoto)akiteta jambo na Dreva Natukunda (kulia mbele) pamoja na Ndugu Abdallah
Gift Disco Sound wakiwa wanachangamsha kwa mziki upokezi huo wa Basi eneo la standi leo hii (mbele) ni Mtangazaji wa kasibante FM ndugu Mbaraka Omari.
Basi lenyewe hili hapa
kwa usafiri wa uhakika tumia mabasi ya Friends.

No comments: