UMOJA WA BAJAJI MBEYA WAAMUA KUZINDUA MPANGO WA KUTEMBELEA WATOTO YATIMA MBEYA
Mwenyekiti wa umoja Bajaji mbeya Bw.Idd Ramadhan |
Katibu wa umoja wa bajaji Mbeya Bw.Ernest Mwaisango
Umoja wa Vijana waendesha Pikipiki za magurudumu matatu Mkoani Mbeya umeamua kuzindua mpango wa kutembelea watoto yatima na kutoa misaada kutokana na faida wanayoipata baada ya kusaijili umoja wao na kuchana na kutumisha kwenye maandamano ya kisiasa na kusababisha vurugu Jijini .
Akizungumza na waandishi wa habari mwenyekiti wa umoja huo Bw.Idd Ramadhan alisema kuwa umoja huo umepata faida kubwa ya kuongeza kipato na kuwa na utulivu baada ya kusajili umoja wao na kuzinduliwa na naibu waziri wa Elimu na Mafunzo ya ufundi Bw.Philip Mulugo na hivyo kuona sababu ya kusaidia watoto yatima.
Alisema lengo kuu la umoja wao wenye wanachama zaidi ya 800 ni kuinuana kiuchumi kwa akuwawezesha vijana kuwa vitega uchumi na kuiondokana na umasiki na kutumia na wanasiasa wasio na mpango wa kusaidia vijana ambapo wamekuwa wakiwatumia wakati wakiwahitaji na kisha kuwaacha baada ya kupata faida wao.
Bw.Ramadhan alisema kuwa kwa kuanza watakuwa wakitembelea watoto yatima kituo kimoja kila mwisho wa mwezi kwa kuwapa mahitaji madogo ya nyumbani ambayo wamekuwa wakiyakosa kwa muda mrefu baada ya kuondokewa na wazazi wao waliokuwa wanawatagemea .
“sisi ni vijana ambao tumeamua kuwa wajasiliamali ambapo tumejipanga kwa ajili ya kuinuana kiuchumi lakini kutokana na faida tunayoipata tumeamua kuwa tutakuwa tunaitumia kwa ajili ya kuwasaidia watoto yatima katika vituo vilivyopo Mbeya na tutazindua mpango huu mwishoni mwa mwezi.”alisema.
Aidha Katibu wa umoja huo Bw.Ernest Mwaisango alisema mbali na kutembelea watoto yatima wamejipanga kwa ajili ya kuhakikisha wanawakusanya vijana ,wamachinga,wapiga debe ,waendesha maroli na makundi mengine ya vijana kwa ajili ya kuwahamasisha kujiunga na kuachana na kutumika katika vurugu zinazoondoa amani ya Mkoa pasipo sababu.
Alisema kuwa vijana wanazo nguvu za kutosha kujituma katika shughuli mbali mbali na hivyo kinachotakiwa kwa serikali ni kuungwa mkono katokana juhudi zao na kisha kuonesha mpango wao unaoweza kuwasaidia kuwakomboa katika maisha ya kutumika na kuiingia katika maisha ya uzalishaji mali na kisha kusaidia wengine wasio jiweza.
Bw.Mwaisango alisema kuwa wameweka mpango kazi katika umoja wao kwa ajili ya kushirikiana na uongozi wa serikali hususani Jiji la Mbeya ili waweze kufanikiwa katika mipango yao inayolenga kubadili kabisa sura ya awali ya vijana wa Mkoa wa Mbeya ambapo ilionekana kuwa kazi yao ni vurugu ambapo sasa wataongoza nchini kw akufanya kazi na kutunza amani na utulivu.
No comments:
Post a Comment