Tuesday, February 12, 2013

1O BORA YA EBSS KUANZA ZIARA MIKOANI IJUMAA HII.

 Kampuni ya simu za mkononi ya Zantel leo imetangaza uzinduzi wa ziara za mikoani kwa wasanii walioshiriki shindano la kuimba la Epiq Bongo Star Search ambapo ziara hiyo itaanzia Dodoma ijumaa hii kwenye ukumbi wa Maisha Club ikifuatiwa na Dar es Salaam.

Meneja Mkuu wa Mawasiliano wa Zantel, Awaichi Mawalla(Pichani katikati) amesema itajumuisha vijana walioingia kumi bora, akiwamo Menina Atick, Nsami Nkwabi, Husna Nassor, Geofrey Levis, Wababa Mtuka, Norman Severino pamoja na mshindi wa milioni hamsini, Walter Chillambo.
  Mshiriki wa shindano la Epiq BSS, Nsami Nkwabi, akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari, anayetazama kushoto ni Meneja Mkuu wa Mawasiliano wa Zantel, Awaichi Mawalla
Mshiriki mwingine, Norman Severino naye akiongea mbele ya waandishi wa habari
Katika ziara hiyo pia, ambayo inafanyika kwa mara ya kwanza toka kuanzishwa kwa mashindano hayo mwaka 2006, wapenzi wa muziki watapata fursa ya kumshuhudia mshindi wa Epiq BSS, Walter Chillambo ambaye atakuwa akizundua wimbo wake siku hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ziara hiyo, Afisa biashara mkuu wa Zantel, Sajid Khan, alisema dhumuni kubwa la ziara hiyo ni kuwajengea vijana hao msingi katika kazi yao ya muziki baada ya shindano la Epiq BSS kuisha.

 ‘Lengo letu kuu la kudhamini Epiq BSS haikuwa kumpa mshindi zawadi, la hasha, bali tulikuwa na mpango madhubuti wa kubadilisha maisha ya vijana hawa kupitia vipaji vyao’ alisema Khan.

 ‘Lakini pia dhumuni la Zantel ni kuonyesha kuwa kwa kufanya uwekezaji sahihi kila kitu kinawezekana, na hakika hilo litajionyesha kwa vijana hawa ambao kwa mara ya kwanza toka mashindano ya BSS yaanzishwe hawajawahi kusaidiwa kwa kiasi hiki’ alisisitiza Khan.
 
Kwa upande wao washiriki watakaokuwa kwenye ziara hiyo wameishukuru kampuni ya Zantel kwa kuwasaidia kurekodi nyimbo zao, kuzitangaza na sasa ziara hii.
 
 ‘Hakika Zantel wameonyesha utofauti na makampuni mengine, kwani makampuni mengi hupotea baada ya kumalizika kwa shindano au tukio husika, ila Zantel wamekuwa nasi baada ya kuisha mashindano wakihakikisha tunarekodi nyimbo zetu na kuzitangaza, tunashukuru sana kwa hilo’ alisema Nsami Nkwabi, mmoja wa washiriki watakaokuwepo kwenye ziara hiyo.
 
Ziara hii pia itawapa fursa kubwa Zantel na washiriki kutoa shukrani kwa mashabiki wa mziki waliowaunga mkono wakati wa mashindano.
 
Kwa upande wake mshindi wa Epiq BSS alisema mashabiki watarajie burudani kali kutoka kwake,‘ nimejipanga sana kwa ajili ya kuwaonyesha watanzania kuwa hawakukokosea kunipigia kura niwe mshindi’ alisema Walter.
 
Wasanii wengine watakaotoa burudani kwenye ziara hii ni Barnaba, Ben Paul, Linah na Ali Nipishe.

No comments: